#repost @jatu_plc

・・・

#RIPOTI YA SIKU YA MWENENDO WA HISA ZA JATU PLC KATIKA SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM (DSE).


Leo 18.12.2020  jumla ya hisa 1700 za JATU PLC zenye thamani ya Tsh 2,448,000 zimeuzwa na kununuliwa katika miamala 8


Bei ya hisa za kampuni zimepanda kutoka Tsh 1,320 ambayo ilikua bei ya ya kufungia Jana na kufika leo Tsh 1,440 bei ya kufungia ,ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 9.09%  kwa siku moja ya mauzo. 


Soko la hisa hadi kufikia siku leo kuna jumla ya oda ya hisa 32,582 zinazosubiriwa kununuliwa.


Thamani ya kampuni imezidi kuongezeka mpaka kufikia Tsh 3.12 Billion ukilinganisha na Tsh 2.86 Billion ya siku ya jana tarehe 17 Desemba, 2020.


Tunaendelea kuwakaribisha kujiunga na kampuni yetu ya JATU PLC kwenye fursa yoyote ya uwanachama ambazo ni :-


▪️Mwanachama mteja ,ambae anajiunga kwa lengo la kununua bidhaa za Jatu tu ili kutengeneza faida gawio la faida kila mwisho wa mwezi kutoka kwenye gawio la faida#kulaulipwe


▪️Mwanachama mkulima, anayejiunga ili kushiriki katika shughuli za kilimo na kampuni ili kulima kisasa na kutengeneza faida kupitia soko la mazao kutoka Jatu.#limanajatubilastress


▪️Mwanachama mwanahisa ambae yeye anajiunga kwa kununua hisa za kampuni na kutengeneza uwekezaji wenye faida kila mwisho wa mwaka(Gawio) au kuendelea kununua na kuuza hisa zake  kwa bei ya juu na kutengeneza kipato.Mwanachama huyu pia anaweza kushiriki kwenye uwekezaji wa miradi ya kilimo na Jatu ili kulima kwa ajili kukifanya  kilimo kuwa sehemu ya biashara.


▪️Mwanachama balozi ambaye anaiwakilisha jatu katika jamii.


//Pia tunawakaribisha kuwekeza katika mradi wa kilimo cha zao la Parachichi unaofanyika mkoa wa Njombe sababu uwekezaji wa  kilimo hiki unafaida kubwa kwenye mavuno na kudumu ndani ya miaka 30 , ni zao lenye thamani kubwa duniani. Mashamba bado yako unakaribishwa kufanya  manunuzi ya shamba mapema kabla ya tarehe 30.12.2020 ili ujiunge na mradi huu rasmi kuanzia mwezi wa kwanza 2021.


//Tunaendelea pia  kusajili mawakala kutoka sehemu mbalimbali na kuendelea kusisiza watu wajitoke ili waweze kujitengenezea ajira ya kidumu kutoka kwenye faida ya mzigo wako wa bidhaa.


By Sarafina Adrian, mchumi na mchambuzi wa maswala ya hisa ,